Kongamano kubwa la wafanyabiashara Afrika Mashariki “East Africa Investment Forum’ linatarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali.
2024-07-03 10:22:32| cri

Mwenyekiti wa Chama cha watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Tanzania (TAFINA), Cynthia Ponera, amesema kongamano hilo kubwa lina lengo la kuunganisha wafanyabisahara hususani watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, na kwenye kuandaa kongamano hilo, wamepata ushirikiano mkubwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambao pia watashiriki.

Amesema kampuni 62 zinatarajiwa kushiriki, ikiwa ni pamoja na washiriki kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kongamano hili litasaidia kuwaleta wawekezaji watakaoangalia fursa za uwekezaji nchini Tanzania.