Serikali ya Tanzania yasisitiza kupiga marufuku kuvua Ziwa Tanganyika
2024-07-04 11:07:30| cri

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu wa Tanzania, Bwana Alexander Mnyeti, amemtaka uamuzi wa serikali wa kufunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika uheshimiwe.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja siku chache baada ya baadhi ya maofisa wa kutumia mikutano ya hadhara kuwatangazia wananchi kuwa wanaruhusiwa kuvua kwa ndoano pembezoni mwa ziwa hilo, na sio kwa nyavu.

Serikali ya Tanzania ilifunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15 mwaka huu kwa lengo kupumzisha ziwa hilo, ili kuwezesha samaki kuzaliana na kuongeza tija kwa wavuvi wanaofanya shughuli zao ziwani humo. 

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu uamuzi huo wa serikali.