Kenya kuboresha ushirikiano na China ili kukuza uchumi wa bluu
2024-07-04 08:42:23| CRI

Waziri wa Madini, Uchumi wa Bluu na Masuala ya Bahari wa nchini Kenya Salim Mvurya amesema, nchi hiyo inatafuta kuboresha uhusiano wake na China ili kukuza uchumi wa kijani.

Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua kando ya mkutano wa siku mbili wa Uwekezaji wa Bluu barani Afrika unaofanyika Kwale nchini Kenya, Waziri Mvurya amesema sekta ya uchumi wa bluu kwa sasa inachukua asilimia 2.5 ya uchumi wa Kenya, na kuongeza kuwa, Kenya inatafuta wenzi wa kimataifa ikiwemo China ili kuendeleza miundombinu ya uvuvi na mambo ya bahari.

Amesema mazungumzo yanaendelea na serikali ya China kuhusu kuongeza ushirikiano wa uvuvi wa baharini, ikiwemo uwezekano wa meli za China kushiriki katika uvuvi kwenye pwani ya Bahari ya Hindi nchini humo.