Watu 14 wauawa katika vurugu zilizotokea kwenye kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Kenya
2024-07-04 08:42:54| CRI

Watu 14 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mapigano makali kati ya makabila mawili yanayopingana kutoka Sudan Kusini katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, iliyoko Kaunti ya Turkana, kaskazini magharibi mwa Kenya.

Meneja wa kambi hiyo Edwin Chabari amesema, mapigano hayo kati ya kabila la Nuer na Anyuak yamesababisha vifo na watu kukimbia makazi yao katika siku nne zilizopita.

Amesema vikosi vya usalama vya Kenya vimepelekwa kwenye kambi hiyo ili kurejesha utaratibu na kuzuia vifo zaidi vya watu na uharibifu wa mali. Pia amesema, maofisa wa huko wameanzisha majadiliano kati ya makabila hayo hasimu ili kuepuka vurugu wakati timu za wahudumu wa afya wakitoa matibabu kwa majeruhi.