Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Astana.
Rais Xi amedokeza kuwa mwezi Januari mwaka huu kwenye ziara ya kiserikali ya rais Mirziyoyev nchini China, waliamua kuinua uhusiano kati ya nchi mbili hadi kufikia ngazi ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kwa hali zote katika zama mpya, na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Uzbekistan katika mwanzo mpya wa juu zaidi.
Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, China inaharakisha maendeleo yake, na Uzbekistan pia inaendeleza kwa kina mkakati wa "Uzbekistan-2030". Pia amesema China inapenda kushirikiana na Uzbekistan kuhimiza maendeleo ya hali ya juu ya uhusiano kwa kuzingatia hatma ya taifa na maslahi ya wananchi.
Rais Mirziyoyev amesema chini ya uongozi wa busara wa Rais Xi Jinping, China imekabiliana na hatari na changamoto mbalimbali na kupata mafanikio makubwa. Uzbekistan inapenda kuratibu na kushirikiana kwa karibu na China katika mifumo ya pande nyingi kama vile Utaratibu wa China-Asia ya Kati na Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai, na kuhimiza utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo Duniani (GDI), Pendekezo la Usalama Duniani (GSI), na Pendekezo la Ustaarabu Duniani (GCI) yaliyotolewa na Rais Xi Jinping.