Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza mipango ya kuanza kufuatilia watoa huduma za fedha kupitia mifumo ya simu za mkononi ambao hawajapunguza gharama kama ilivyoainishwa katika waraka uliotolewa na serikali mapema mwaka huu.
Mchambuzi wa mifumo ya programu za kompyuta wa BoT, Bw. Octalion Urassa, amesema hadi sasa benki 39 za kibiashara na makampuni sita ya simu, wamejiunga na mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao. Hata hivyo hakusema nini kitafanywa dhidi ya taasisi za fedha zitakazobainika kwenda kinyume Maagizo ya BoT.
Amesema hapo awali, walianza na mradi wa majaribio kwa kuhusisha benki chache za biashara na kampuni moja ya simu, lakini sasa wote watoa huduma wameunganishwa kwenye mfumo huo.