Tanzania na Msumbiji Kuunda Umoja wa Wazalishaji wa Korosho Afrika
2024-07-04 11:09:05| cri

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, ametangaza kuwa Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kuunda umoja wa wazalishaji wa korosho Afrika, ili kuwa na sauti moja katika masoko ya kimataifa.

Rais Samia amesema Msumbiji na Tanzania wote ni wazalishaji wa korosho, lakini si wapangaji wa bei ya korosho, umoja huo utawasaidia kuwa na sauti kwenye upangaji wa bei ya korosho duniani.

Rais Samia amefafanua kuwa moja ya mikakati ni kuhakikisha kuwa wale wanaonunua korosho ndani ya nchi wanapata bei nzuri, na hivyo kuchochea uzalishaji na kuongeza kipato kwa wakulima. Katika juhudi za kujenga ushirikiano huu, Rais Samia amesema pia walikubaliana Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embaló kuhusu wazo hilo alipolitembelea Tanzania. 

Umoja huu unatarajiwa kusaidia nchi za Afrika zinazozalisha korosho kuwa na ushawishi zaidi katika masoko ya kimataifa, na hivyo kuboresha bei na faida kwa wakulima wa korosho katika bara hili.