Hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa mradi wa ukarabati wa barabara nchini DRC unaotekelezwa na kampuni ya China yafanyika mjini Kananga
2024-07-04 11:06:24| cri

Sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ukarabati wa barabara unaotekelezwa na kampuni ya China nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefanyika Kananga katika jimbo la Central Kasai nchini humo.

Waziri wa mambo ya miundombinu na ujenzi wa umma wa DRC Bw. Alexis Gisaro Muvuni amesema kwenye sherehe hiyo kwamba barabara hiyo inabeba matarajio ya kuleta fursa za maendeleo kwa watu wa jimbo hilo na ushiriki wa upande wa China umewezesha mpango wa DRC wa muunganisho wa barabara katika mambo ya fedha na teknolojia.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Miundombinu ya China na Congo, Pang Long, akiwakilisha upande wa makampuni za China zilizoshiriki kwenye mradi huo, amesema barabara hiyo yenye urefu wa takriban kilomita 230, inayounganisha Kananga na Kalamba Mbuji, inatarajiwa kurahisisha usafirishaji na biashara ya kuvuka mipaka kwa nchi ya DRC.