UNICEF: Duru mpya ya mapambano huko Al-Fashir nchini Sudan imesababisha vifo na majeruhi kwa watoto zaidi ya 400
2024-07-04 13:51:57| cri

Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Adele Khodr amesema msikiti ulioko kwenye mji wa Al-Fashir jimboni Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan tarehe 1 ulishambuliwa kwa droni, ambapo watoto wasiopungua wanane wameuawa, ikiwa ni pamoja na mtoto wa miezi 18, na watoto wengine tisa wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Tangu duru mpya ya mapambano mjini Al-Fashir ilipolipuka mwezi Mei mwaka huu, watoto zaidi ya 400 wa huko wamejeruhiwa au kuuawa. Khodr amesisitiza ulazima wa kusimamisha madhara kwa watoto, na kutoa wito kwa pande hasimu za Sudan zichukue hatua za kuwalinda watoto mara moja, na kusitisha mashambulizi dhidi ya raia, vifaa vya kiraia na maeneo yenye watu wengi.