Watu 15 wameuawa na wengine 32 kujeruhiwa katika shambulizi la risasi lililofanywa jana na wanajeshi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kwenye soko huko El Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini Magharibi mwa Sudan.
Mkurugenzi mkuu wa Wizara ya afya ya Jimbo la Darfur Kaskazini, Bw. Ibrahim Khatir alisema, shambulio hilo lililenga soko la Al-Mawashi sehemu ya mifugo, na kwamba watu wote waliouawa na kujeruhiwa ni raia.
Tangu tarehe 10 mwezi Mei, mapigano makali yametokea mjini El Fasher, mji mkuu wa mkoa wa Darfur Kaskazini, na ni mapigano makali ya hivi karibuni kati ya Jeshi la Sudan na kikosi cha RSF nchini Sudan yaliyoanza mwezi April, mwaka jana.