UM wasema eneo la Pembe ya Afrika linahitaji dola za kimarekani bilioni 9.8 za msaada wa kibinadamu
2024-07-05 11:50:46| cri



Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) jana imetoa ripoti ikisema, kanda ya Pembe ya Afrika inahitaji dola za kimarekani bilioni 9.8 kwa ajili ya msaada wa kibinadamu.

OCHA imesema nchi za Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini, Somalia, Kenya na Burundi zinahitaji zaidi msaada huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), watu milioni 66.7 katika kanda hiyo wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula na wanahitaji msaada wa kibinadamu.