Rais wa China akutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
2024-07-05 10:42:27| cri

Rais Xi Jinping wa China amekutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres mjini Astana, Kazakhstan wakati akihudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).   

Rais Xi amesema wakati dunia ikikabiliana na mabadiliko ya kasi na binadamu wakikutana na changamoto pamoja na fursa isiyo kifani, kazi ya Umoja wa Mataifa inaweza tu kuimarishwa badala ya kudhoofishwa. Amesema China siku zote itashiriki katika uhusiano wa pande zote na kuunga mkono shirika hilo lichukue nafasi muhimu katika mambo ya kimataifa.

Rais Xi amesisitiza kuwa China inaunga mkono mkutano wa UM juu ya ujenzi wa mustakbali wa dunia (Summit of the Future) na kutarajia mkutano huo kutoa ishara nzuri ya kushikilia uhusiano wa pande nyingi na kuimarisha mafungamano na ushirikiano na kuhimiza usimamizi wa dunia kufuata mwelekeo wa haki na halali zaidi. Pia China inaunga mkono shirika hilo katika juhudi zake za kuchukua nafasi muhimu katika kuhimiza mageuzi ya mfumo wa kifedha wa kimataifa na usimamizi wa akili bandia duniani.

Bw. Guterres ameishukuru China kwa kuunga mkono na kazi ya Umoja wa Mataifa, kutekeleza mfumo wa pande nyingi na kufanya kazi ya kiujenzi katika kuhimiza maendeleo na amani duniani. Amesema Umoja wa Mataifa unatarajia kuzidisha mawasiliano na ushirikiano na China.