Watu 25 wamekufa maji walipokuwa wakikimbia mapigano ya kijeshi yanayoendelea katika Jimbo la Sinnar katikati mwa Sudan baada ya mashua yao ya mbao kupinduka.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, zaidi ya watu 55,400 wamekimbia Singa, mji mkuu wa jimbo la Sinnar, tangu mapigano kati ya Jeshi la Sudan na kikosi cha RSF kuenea sehemu mbalimbali nchini humo mwezi Juni.
Katika ripoti yake ya mwezi Juni, Ofisi hiyo imesema mapigano yaliyoanza katikati ya mwezi April, 2023 nchini Sudan yamesababisha vifo vya watu 16,650.