Rais wa Nigeria achaguliwa tena mwenyekiti wa ECOWAS, na kurejea wito wa kuunda jeshi la kikanda
2024-07-08 08:20:34| CRI

Rais Bola Tinubu wa Nigeria ametoa wito kwa viongozi wa Afrika Magharibi kufanya kazi pamoja ili kuanzisha na kudumisha kikosi cha kikanda cha kukabiliana na matishio ya usalama yanayoongezeka katika eneo la Afrika Magharibi.

Akizungumza mjini Abuja kwenye ufunguzi wa kikao cha 65 cha kawaida cha Mamlaka ya Wakuu wa Nchi na Serikali ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Rais Tinubu, ambaye kwa kauli moja alichaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, amesisitiza kuhusu utendaji wa kikosi hicho, na kuzitaka nchi wanachama kujitolea zaidi kutoa rasilimali zinazohitajika kulinda eneo hilo.

Rais Tinubu pia amesema mpango wa Utekelezaji wa Kikanda wa mapambano dhidi ya ugaidi, umeimarisha ushirikiano katika mafunzo, kupeana taarifa za kijasusi, na uingiliaji kati wa kibinadamu.