Ukame unaosababishwa na El-Nino wapunguza pato la taifa la Botswana kwa asilimia 38
2024-07-08 09:04:58| CRI

Shirika la kufuatilia mabadiliko ya tabianchi la Botswana (BCCN) katika ripoti yake ya hivi karibuni limesema ukame unaosababishwa na athari za El-Nino wakati wa msimu wa mazao wa 2023/2024 umepunguza pato la taifa la Botswana (GDP) kwa asilimia 38.

Ripoti hiyo imesema mavuno ya mazao yamepungua kutoka tani 206,572 za msimu wa mazao 2021/2022 hadi tani 125,184 msimu wa mazao wa 2022/2023, na uzalishaji wa nafaka ukiwa asilimia 23 ya mahitaji ya kitaifa.

Shirika hilo limesema ukame huo unakuja kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yanaongeza joto la maji ya bahari na kubadilisha kiasi cha mvua duniani, na kusababisha ukame na mafuriko yanayoharibu mazao na kuwaua mifugo.