Maofisa wa China na Ethiopia wasisitiza haja ya kukumbatia anuwai ya staarabu kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia
2024-07-08 08:05:36| CRI

Maofisa wa China na Ethiopia wamesisitiza haja ya kuheshimu na kukumbatia anuwai ya staarabu ili kuhimiza amani, maelewano, mahusiano kati ya watu na maendeleo kote duniani.

Wito huo ulitolewa kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu yaitwayo “Mfululizo ya Mihadhara kuhusu Ustaarabu”, yaliyofanyika Jumamosi mjini Addis Ababa. Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa jamii za kiraia kati ya China na Ethiopia.

Akiongea kwenye mazungumzo hayo, naibu mwenyekiti wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kimataifa kwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya China, Li Jun, amesema ni muhimu kueneza maadili ya pamoja ya binadamu ili kuhimiza watu na staarabu tofauti kuwepo pamoja kwa amani.

Naye kamishna wa Jumuiya ya Mazungumzo ya Kitaifa ya Ethiopia, Yonas Adaye amesema mazungumzo hayo ni muhimu katika kudumisha amani na maendeleo ya dunia kupitia mawasiliano na ushirikiano kati ya tamaduni.