Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa Baraza la Maendeleo ya Kijani la Nchi wanachama wa SCO
2024-07-08 14:30:11| cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Baraza la Maendeleo ya Kijani la Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).

Katika barua hiyo, rais Xi amesema kulinda mazingira ya kiikolojia na kuhimiza maendeleo ya kijani, ni maoni ya pamoja ya nchi wanachama wa SCO. Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikishikilia kithabiti dhana ya kuzingatia usafi wa mazingira, na kufuata bila kuyumbayumba njia ya maendeleo ya ustaarabu yenye uwiano kati ya maendeleo ya viwanda, maisha bora na mazingira mazuri ya ikolojia, na kupata mafanikio katika ujenzi wa China Nzuri. Rais Xi pia amesisitiza kuwa China ina matumaini kuwa, kupitia baraza hilo, itaimarisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta ya maendeleo ya kijani, kusaidia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii ya nchi zote wanachama na kuhimiza binadamu na mazingira asili kuishi pamoja kwa masikilizano.