Wimbi la joto lazidisha machungu kwa watu wa Sudan wakati migogoro ikiendelea nchini humo
2024-07-08 09:00:32| CRI

Uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini Sudan umepungua wakati nchi hiyo ikikumbwa na wimbi la joto, ambalo limezidisha machungu kwa watu wa Sudan wanaoteseka na migogoro nchini humo.

Kwa mujibu wa wakulima wa Sudan, uzalishaji wa mahindi nchini humo umepungua kwa zaidi ya nusu kutokana na joto kali ambalo limepita nyuzi 50.

Mashirika ya kimataifa yameonya kuwa mabadiliko ya tabia nchi pamoja na mapigano yanayoendelea nchini Sudan, vimeathiri vibaya sekta ya kilimo na kusababisha uhaba wa chakula unaoweza kuleta baa la njaa nchini humo.