John Cena atangaza kustaafu kucheza mieleka
2024-07-08 22:53:44| cri

Muigizaji na mwanamieleka wa Marekani John Cena ametangaza kustaafu kushiriki mashindano ya mieleka duniani World Wrestling Entertainment (WWE).

Cena alitoa tangazo la kushtukiza kwa mashabiki wakati alipotokea kwenye hafla ya “WWE Money in the Bank” nchini Canada.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 47, ambaye aliingia katika uigizaji miaka 18 iliyopita, alisema shindano lake la mwisho la ulingoni litakuwa 2025 kama sehemu ya ziara ya kuaga.

Cena mara nyingi anachukuliwa kuwa mmoja wa wanamieleka wa kulipwa wa wakati wote na alipata ubingwa wa dunia mara 16 tangu ajiunge na WWE mwaka 2001.

"Leo usiku natangaza rasmi kustaafu kwangu katika WWE," aliwaambia mashabiki wa Toronto ambao walijibu kwa mshangao na baadaye kusema "asante Cena".