Uhalifu kwa vijana na namna ya kuzuia
2024-07-26 08:00:00| CRI

Kijana ni nguvu kazi muhimu katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kutumia akili au nguvu bila ya kusukumwa na mtu yeyote. Kijana katika umri huu anapaswa kujitambua zaidi kwa kutimiza wajibu umpasao kuutimiza ili kuleta maendeleo au mabadiliko. Lakini katika kipindi hiki kama hawakupata muongozo mzuri, baadhi ya vijana hujikuta wakitumbukia kwenye mambo mengi mabaya yakiwemo wizi, ujambazi, kutumia dawa za kulevya ama hata kuwa wauaji. Tumeaminishwa kwa kipindi kirefu sana juu ya umuhimu wa kijana katika taifa linaloendelea.

Tunaelezwa kuwa kijana ni nguvu ya taifa la sasa na lijalo, na kuwa ni juu ya kijana kuendeleza taifa lake. Katika bara la Afrika idadi kubwa ya watu wake ni vijana wa umri chini ya miaka 45, na ni wengi zaidi ikilinganishwa na mabara mengine. Kwa maana hiyo tunaweza kusema kuwa, sehemu ambayo ina changamoto kubwa ya kuhakikisha vijana wake wanapatiwa mwongozo mzuri na mahitaji yao katika jamii ikiwemo kupata elimu ajira na maisha mazuri ili wasije wakapotoka ni bara la Afrika. Lakini je vijana waliopotoka tunawarejesha vipi kwenye mstari ulionyooka? Hii ndio mada yetu kwenye kipindi cha Ukumbi wa wanawake leo hii.