Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bw. Therese Kayikwamba Wagner amesema DRC itashiriki katika juhudi za kidiplomasia wakati na baada ya usitishwaji vita wa kibinadamu na kundi la M23, ambalo limetwaa sehemu kubwa ya mashariki mwa nchi hiyo.
Usitishwaji vita huo wa siku 14, kuanzia Julai 5 hadi 19, unajumuisha njia iliyowekwa kwa ajili ya kurejea kwa amani mashariki mwa nchi hiyo.
Waziri huyo amesema usitishwaji vita haumaanishi kuwa serikali inaacha kuwa macho, akisema juhudi za kidiplomasia zinalenga "suluhisho la kudumu" la kurejesha amani.