China yaitaka Marekani iache kuichafua na kuchangia usalama wa mtandao
2024-07-09 13:51:33| cri

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lin Jian jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, China imeitaka Marekani iache kuichafua na kuchukua hatua za kuwajibika, ili kutoa mchango kwa ajili ya amani na usalama wa mtandao.

Ripoti iliyotolewa karibuni na Kituo cha Kitaifa cha Kukabiliana na Virusi vya Kompyuta cha China, Maabara ya Kitaifa ya Teknolojia ya Kuzuia Virusi vya Kompyuta na Kampuni ya Usalama ya Dijitali 360 ilionesha kuwa, tangu mwaka 2023 Marekani imekuwa ikitangaza kwa kiasi kikubwa shirika la wadukuzi lijulikanalo kama "Volt Typhoon", na kujishughulisha na kampeni ya kutoa taarifa potofu dhidi ya China duniani.