Madaktari wa China, UNESCO watoa huduma za matibabu bila malipo kwa kituo cha watoto yatima nchini Ghana
2024-07-09 08:33:38| CRI

Kikundi cha 13 cha madaktari wa China nchini Ghana kimeshirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kutoa huduma za matibabu bila malipo kwa watoto yatima 61 katika Kituo cha Motherly Love Orphanage huko Kwabenya, mjini Accra, Ghana.

Watoto hao wenye umri wa miaka minne hadi 21, walifanyiwa upimaji wa afya. Zhang Rijia, mkuu wa kikundi cha madaktari wa China alisema watoto hao wanahitaji msaada wa kimatibabu, na wanafurahia kupata fursa ya kuwatembelea na kutoa huduma za kimsingi za afya.

Mwakilishi wa UNESCO nchini Ghana Edmond Moukala amesema hatua hii inaonyesha kivitendo kwa hatua inayochukuliwa kujenga kikamilifu jamii yenye amani na usawa. Ofisa mkuu mtendaji wa kituo cha watoto yatima Bw. John Azuma, alitoa shukrani kwa madaktari wa China na wale wa UNESCO.