Guinea-Bissau yapongeza mchango wa China katika maendeleo ya nchi hiyo
2024-07-09 08:38:01| CRI

Rais Umaro Embalo wa Guinea-Bissau amesema China ni mshirika muhimu katika ushirikiano wa pande mbili, na kushukuru mchango wa China katika maendeleo ya nchi hiyo.

Rais Embalo alisema hayo kwenye mkutano na wanahabari katika uwanja wa ndege wa Bissau kabla ya kuanza safari yake nchini China. Pia amesema nchi hizo mbili zimekuwa washirika wa jadi tangu kuanza kwa mapambano ya ukombozi wa Guinea-Bissau.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Rais Embalo atafanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 13 mwezi Julai kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping.