Wataalamu waitaka EAC kukubali Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kikanda
2024-07-09 09:06:23| CRI

Wataalamu wamerejea tena mwito kwa baraza la mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuharakisha marekebisho ya Mkataba wa EAC kuiwezesha lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kanda hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na makao makuu ya Jumuiya ya EAC huko Arusha, wataalamu wamewataka nchi zote wanachama kutunga sheria ya kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli iliyofanyika huko Mombasa.

Waziri wa jinsia, utamaduni, sanaa na urithi wa Kenya Bi. Aisha Jumwa amesema, Kiswahili ni lugha ya umoja katika kanda hiyo, inayotumiwa na watu zaidi ya milioni 200. Amezihimiza zote nchi wanachama wa EAC kuhimiza sheria na sera ziandikwe na zichapishwe kwa lugha ya Kiswahili.