Faith Kipyegon wa Kenya avunja rekodi yake ya dunia ya mbio za mita 1,500 mjini Paris
2024-07-09 11:00:04| cri

Bingwa mara nyingi wa Olimpiki na dunia wa mbio za mita 1,500, Faith Kipyegon wa Kenya, amevunja rekodi yake ya dunia ya mbio za mita 1,500 katika Ligi ya Diamond ya Paris.

Kipyegon, bingwa mara mbili wa Olimpiki wa mbio za mita 1,500, jana alifuta rekodi yake ya awali aliyoiweka zaidi ya mwaka mmoja uliopita kwa sekunde 0.07 aliposhinda mbio zake kwa dakika tatu na sekunde 49.04 katika mzunguko wa nane wa Ligi ya Diamond.

Kipyegon aliweka rekodi ya dunia kwa mara ya kwanza Juni 2, mwaka jana mjini Florence, Italia, akishinda kwa kutumia muda wa saa 3:49.11 na kufuta rekodi ya awali ya saa 3:50.07 iliyowekwa na Muethiopia Genzebe Dibaba Julai 17, 2015.

Jumapili, Julai 7, alivunja rekodi yake mwenyewe katika mbio hizohizo ambapo alivunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 5,000 ya saa 14:06.62, ambayo ilikuwa imewekwa na Letesenbet Gidey wa Ethiopia mjini Valencia Oktoba 7, 2020 Muethiopia huyo alipokimbia kwa saa 14:05.20.