Zimbabwe yatafuta kuimarisha ushirikiano na China kwenye sekta ya sanaa
2024-07-10 08:18:07| CRI

Mkurugenzi wa Baraza la Kitaifa la Sanaa la Zimbabwe (NACZ), Napoleon Nyanhi amesema, Zimbabwe inatafuta kuimarisha ushirikiano na China kwenye sekta ya sanaa za kiuvumbuzi ili kukuza sekta hiyo na kuhimiza uhusiano wa kiutamaduni kati ya pande hizo mbili.

Akihojiwa na shirika la habari la China Xinhua kando ya Jukwaa la kwanza la Harare kuhusu Wiki ya Afrika na Taaluma, Bw. Nyanhi amesema mawasiliano mengi yamefanyika kwenye sanaa za maonesho, kama vile muziki, ngoma na upigaji wa ala, Zimbabwe inatarajia ushirikiano zaidi na China kwenye maeneo mengine ya sanaa, ikiwemo ubunifu wa mitindo, utengenezaji wa filamu na vipindi vya televisheni.

Bw. Nyanhi pia amelitaja shindano la Dreamstar lililofadhiliwa na China, ambalo ni shindano kubwa zaidi la aina yake kutafuta vijana wenye vipaji nchini Zimbabwe, kuwa lina umuhimu mkubwa katika kuwahamasisha wasanii wa fani mbalimbali nchini humo.