Moody's yashusha makadirio ya uwezo wa Kenya kulipa madeni baada ya serikali kuachana na mswada wa kodi
2024-07-10 08:48:08| CRI

Shirika la kimataifa la ukadiriaji Moody's limepunguza makadirio kuhusu uwezo wa Kenya kulipa mikopo, likitaja "kupungua kwa uwezo wa kudumisha makusanyo ya fedha yanayotegemea mapato ambayo yangeboresha uwezo wa kumudu madeni na kuliweka deni kwenye hali ya kushuka.

Moody’s lilishusha daraja la Kenya katika ukadiriaji wa watoaji wa muda mrefu wa fedha za kigeni na ukadiriaji wa  madeni yasiyolindwa ya kigeni hadi "Caa1" kutoka "B3".

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Rais William Ruto wa Kenya kulazimika kuondoa mpango mpya wa utozaji kodi katika Mswada wa Fedha wa 2024 kufuatia wiki tatu za maandamano ya umma.