Idadi ya watu nchini Senegal yapita milioni 18 mwaka 2023
2024-07-10 09:18:10| CRI

Takwimu zilizotolewa na shirika la taifa la takwimu na idadi ya watu la Senegal, zinaonesha kuwa idadi ya watu nchini Senegal kwa mwaka 2023 imeongezeka na kufikia 18,126,390.

Takwimu zinaonyesha kuwa takriban asilimia 50.6 ya watu ni wanaume na asilimia 49.4 ni wanawake, asilimia 75 wana umri wa chini ya miaka 35, karibu nusu wana umri wa chini ya miaka 19, na asilimia 39 wana umri wa chini ya miaka 15.

Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2023, idadi ya watu nchini Senegal iliongezeka kwa asilimia 2.9 kwa mwaka, na kwa kasi hiyo, idadi ya watu inaweza kuongezeka maradufu ndani ya miaka 25.