Naibu waziri mkuu wa China asema China inapenda kuhimiza ujenzi wa kisasa na Afrika
2024-07-10 09:21:36| CRI

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu Guozhong amesema, China inapenda kutoa fursa mpya kwa Afrika kuhusu maendeleo yake na kushikana mikono katika kuhimiza ujenzi wa kisasa.

Bw. Liu ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisiti cha China, amesema hayo kwenye hafla ya ufunguzi ya Mkutano wa 5 wa Baraza la Ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa za China na Afrika iliyofanyika mjini Guangzhou.

Bw. Liu amesema China na Afrika zimefanya juhudi kwa pamoja kuimarisha na kuzidisha uhusiano na pande mbili zimeingia katika hatua mpya ya ujenzi wa jumuiya ya ngazi ya juu yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya.