Kenya yahimiza ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi ili kuimarisha utalii wa adventure
2024-07-10 08:48:49| CRI

Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) imesema inatumia ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ili kuchochea fursa za utalii wa  adventure nchini Kenya.

Ofisa Mkuu mtendaji wa KTB Bibi June Chepkemei amesema utalii wa adventure umeonesha uthabiti na uwezo wa kukaribisha watalii zaidi nchini Kenya. Utalii huu licha ya kuwa endelevu pia una uwezo wa kuunga mkono uchumi wa wenyeji

Ametaja uzoefu anuwai wa utalii wa aina hiyo kuwa ni pamoja na kutazama wanyama kwa njia rafiki kwa mazingira, kuwatazama ndege, kupanda milima na michezo ya kwenye maji.