Jukumu la Majaji na Mahakimu Wanawake katika kuleta haki
2024-07-12 08:15:43| CRI

Mkutano wa Tatu wa Wajumbe Wote wa Awamu ya 20 ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) utafanyika Julai 15 mwaka huu nchini China. Katika Mkutano wa Tatu wa Wajumbe Wote wa Awamu ya 11 ya CPC uliofanyika mwezi Desemba mwaka 1978, sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China ambayo ina umuhimu mkubwa wa kihistoria ilianzishwa.

Mwaka 2001 China ilifanikiwa kujiunga na Shirika la Biashara Duniani (WTO). Hayo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana baada ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ianze kutekelezwa, ambayo yameonesha ushiriki wa China katika utandawazi wa kiuchumi duniani. Kuanzia hapo, China imeanza kubeba jukumu kubwa zaidi katika jukwaa la kimataifa. Katika mchakato wa mazungumzo ya kujiunga na shirika hilo ambao ni mgumu tena ulichukua muda mrefu, kuna mwanamke mmoja wa China aliyeshiriki mchakato mzima na pia kufanya juhudi kubwa. Yeye ni Bibi Zhang Yuejiao ambaye alikuwa rais wa Baraza la Rufaa la Shirika la Biashara Duniani (WTO).

Hivi sasa wanawake wengi kama Zhang Yuejiao wanafanya bidii katika mambo ya majaji duniani. Hivyo Leo katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake tutaelezea hadithi ya mwanamke huyo shupavu Zhang Yuejiao na mchango unaotolewa na wanawake hodari duniani katika mambo ya majaji.