Botswana kuwa mwenyeji wa mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi zinazoendelea zisizo na bandari
2024-07-11 09:16:22| CRI

Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi zinazoendelea zisizo na bandari utafanyika mwezi wa Desemba nchini Botswana.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kuhusu “Mitindo Zaidi ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nchi Zinazoendelea zisizo na Bandari”, likikubali ombi la Botswana kuwa mwenyeji kuanzia Desemba 10 hadi 13.

Baraza kuu la Umoja huo limeamua kaulimbiu ya mkutano huo kuwa “kuhimiza maendeleo kupitia uhusiano wa kiwenzi”, huku likiitia moyo serikali, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, makundi makuu na wafadhili wengine kuchangia mfuko kuunga mkono maandalizi ya mkutano huo na ushiriki wa nchi zinazoendelea zisizo na bandari.