Makamu wa rais wa Zambia Bibi Mutale Nalumango amesema washirika wameipa Zambia takriban dola milioni 511 za Marekani ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na ukame.
Gazeti la Zambia Daily Mail limemnukuu Bibi Nalumango akisema watu milioni 6.6 wanahitaji chakula cha msaada nchini Zambia, na madhumuni ya msaada huu na ule kutoka kwa watu wengine wenye njia njema, ni kusaidia serikali kuhakikisha wazambia hawafi kwa njaa.
Makamu huyo wa rais amesema amezuru sehemu kadhaa za nchi zilizoathiriwa na ukame ili kutathmini athari za hali hiyo, na kusema kuwa baadhi ya mashamba hayana mavuno kabisa.