China yatoa waraka kuhusu “Ulinzi wa Mazingira ya Kiikolojia ya Bahari ya China”
2024-07-11 11:07:07| CRI

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China leo tarehe 11 imetoa waraka kuhusu “Ulinzi wa Mazingira ya Kiikolojia ya Bahari ya China”.

 

Mbali na utangulizi na hitimisho, waraka huo una sehemu saba zikiwa ni pamoja na kujenga mazingira ya kiikolojia ya bahari yenye masikilizano kati ya binadamu na bahari, kuhimiza ulinzi wa mazingira ya kiikolojia ya bahari, kusimamia mazingira ya kiikolojia ya bahari, kufanya ulinzi na kurejesha mazingira ya kiikolojia ya bahari kwa njia ya kisayansi, kuimarisha usimamizi wa mazingira ya kiikolojia ya bahari, kuinua kiwango cha maendeleo ya kijani ya bahari yanayotoa kaboni chache, na kuanzisha kwa pande zote ushirikiano wa kimataifa katika kulinda mazingira ya kiikolojia ya bahari.  

Waraka huo umesema, China ni mhamasishaji na mtekelezaji wa ulinzi wa mazingira ya bahari, na kulinda vizuri hali ya kiikolojia ya bahari kunahusiana na ujenzi wa China Nzuri na nchi yenye nguvu kubwa ya bahari. Katika miaka mingi iliyopita, China imekuwa ikitoa kipaumbele katika ulinzi wa mazingira ya kiikolojia na usimamizi wa mazingira, kuratibu uhusiano kati ya maendeleo na ulinzi wa mazingira, kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu kwa kufuata msingi wa kiwango cha juu cha ulinzi wa mazingira, ili kujitahidi kujenga mazingira ya bahari yenye masikilizano kati ya binadamu na bahari.