Mradi wa maboresho ya barabara unaotekelezwa na kampuni ya China nchini DRC wawekwa jiwe la msingi
2024-07-11 09:00:22| CRI

Sherehe ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ukarabati na maboresho ya barabara ya taifa ya N1 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) imefanyika jana Jumatano katika jimbo la Lualaba, kusini-mashariki mwa nchi hiyo, ukiwa ni moja ya miradi ya ushirikiano kati ya China na DRC.

Waziri wa miundombinu na ujenzi DRC Alexis Gisaro Muvuni alipohutubia sherehe hiyo amezipongeza kampuni za China kwenye mradi huo, na kusema chini ya ushirikiano huo, miradi mingi ya miundombinu imezinduliwa, ukiwemo mradi wa barabara za mzunguko mjini Kinshasa, na inatarajiwa kutoa mchango mkubwa kwa jamii.

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Miundombinu ya China na DRC Pang Long, amesema kwa niaba ya kampuni za China zilizoshiriki kwenye miradi ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kuwa mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa takriban kilomita 900 umefungua musktabali mpya wa ushirikiano wa nchi hizo mbili na ameahidi kushirikiana kwa karibu na DRC kukamilisha mradi huo.