Karakana ya Luban kwenye Chuo Kikuu cha Machakos nchini Kenya inaendelea kutoa mafunzo katika vikundi vya watu sita, kuhusu namna ya kuunganisha sehemu mbalimbali za kompyuta.
Karakana hiyo ni moja ya idara muhimu katika Chuo Kikuu cha Machakos ambayo makumi ya wanafunzi wanapata mafunzo kila siku. Chuo Kikuu cha Machakos kilianzisha karakana hiyo mwaka wa 2019 kwa msaada kutoka kampuni kubwa ya teknolojia ya China Huawei na Chuo cha Ufundi cha Mji wa Tianjin (TCVC).
Wanafunzi katika karakana hiyo wamekuwa wakiipongeza karakana hiyo kwa kuchochea hisia na upendo kwa taaluma wanazosoma.