Benki kuu ya Ethiopia (NBE), imetangaza kupitishwa kwa sera ya fedha yenye msingi wa viwango vya riba na taratibu bora za kimataifa, ili kuhakikisha uthabiti wa bei na kukuza ukuaji wa uchumi.
Utaratibu huo mpya unakuja wakati benki hiyo imechukua hatua ya kuachana na sera ya awali ya ukomo wa mikopo ili kudhibiti mfumuko wa bei.
Kwa sasa benki hiyo imeweka kiwango cha riba cha awali kuwa asilimia 15, na itatumia sera mpya ya viwango vya riba, kama njia ya kuunda soko baina ya benki kwa ajili ya biashara ya fedha na kuwa na athari pana kwenye mazingira ya mambo ya fedha na mikopo.
Kuanzia Julai 11, Benki hiyo inaanzisha minada inayohusiana na sera ya fedha ili kuondoa ukwasi kutoka au kuongeza ukwasi kwenye mifumo ya benki kila baada ya wiki mbili.