DRC yapongeza kituo cha kuzalisha umeme kwa maji kilichojengwa na China
2024-07-12 08:39:42| CRI

Waziri wa miundombinu na ujenzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bw. Alexis Gisaro Muvuni, amesema anafurahishwa na mbinu zinazotumiwa katika uendeshaji wa kituo cha kuzalisha umeme kwa maji cha Busanga katika jimbo la Luabala kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Bw. Muvuni amesema DRC na China zinapaswa kuhimiza uwekezaji katika uzalishaji wa umeme na miundombinu, na kuibua uwezekano katika ushirikiano kwenye uzalishaji wa umeme kwa maji na nishati ya jua.

Mwezi Oktoba 2023, Rais Felix Tshisekedi wa DRC alizindua kituo hicho na kuanzisha uzalishaji wa umeme katika kituo hicho. Kituo hicho kimewekezwa na kujengwa kwa pamoja na makampuni ya China.