Lesotho yasema itaendelea kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja
2024-07-12 09:06:52| CRI

Mfalme Letsie III wa Lesotho amesema Lesotho inatilia maanani kuendeleza uhusiano kati yake na China na itaendelea kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, kuimarisha ushirikiano halisi katika sekta mbalimbali na kusukuma mbele uhusiano kati ya pande hizo mbili.

Mfalme Letsie III amesema hayo jana wakati akipokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa China nchini Lesotho Bw. Yang Xiaokun, na kushukuru msaada na uungaji mkono wa China kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Lesotho.

Bw. Yang Xiaokun ameishukuru Lesotho kwa kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kupenda kushirikiana na Lesotho kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.