Wafungwa watoroka kutoka kwenye gereza linaloshikilia wanamgambo nchini Niger
2024-07-12 08:26:56| CRI

Wizara ya mambo ya ndani ya Niger imesema, baadhi ya wafungwa jana Alhamisi walitoroka kutoka kwenye gereza linaloshikilia wanamgambo mkoani Tillabery magharibi mwa nchi hiyo.

Wizara hiyo haikutaja idadi ya wafungwa waliotoroka na jinsi walivyotoroka kutoka gereza la Koutoukale, lililoko kilomita 50 kaskazini magharibi kutoka kwa Niamey.

Gereza hilo linashikilia wanachama wengi wa kundi la Boko Haram na makundi mengine ya Sahel.

Mamlaka za huko zimeweka marufuku ya kutoka nje usiku kwenye eneo la Tillabery, lakini hazijatoa maelezo zaidi.