Umoja wa Mataifa wakadiria idadi ya watu duniani itafikia kilele ndani ya karne hii
2024-07-12 10:23:33| CRI

Umoja wa Mataifa umetoa ripoti ikikadiri kuwa idadi ya watu duniani itafikia kilele ndani ya karne hii.

Kwa mujibu wa ripoti kuhusu Makadirio ya Idadi ya Watu 2024, idadi ya watu duniani itafikia kilele katikati ya miaka ya 2080, ikiongezeka kutoka watu bilioni 8.2 wa mwaka 2024, hadi bilioni 10.3 katikati ya miaka ya 2080, na kurudi kuwa bilioni 10.2 hivi hadi kufikia mwishoni mwa karne hii.

Kiasi cha idadi ya watu duniani mwaka 2010 kinakadiriwa kupungua kwa asilimia 6 ama milioni 700 kuliko mungo uliopita.

Kulingana na ripoti hiyo, kilele cha awali cha idadi ya watu kinatokana na vyanzo kadhaa, ikiwa ni pamoja na viwango vya chini vya uzazi katika baadhi ya nchi kubwa duniani.