Idadi ya vijana nchini Uganda ni kichocheo kikuu cha ongezeko la uchumi na mabadiliko
2024-07-12 08:39:06| CRI

Wakati dunia imeadhimisha Siku ya Idadi ya Watu, takwimu za hivi karibuni za Uganda zinaonesha kuwa, wataalam wamesema idadi ya vijana inayoongezeka nchini humo ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi na mabadiliko.

Takwimu za awali zilizotolewa mwezi uliopita na shirika la takwimu la Uganda baada ya sensa ya sita nchini humo, zinaonyesha kuwa idadi ya watu nchini Uganda imefikia milioni 45.9, kati yao asilimia 73 wana umri wa chini ya miaka 30.

Wataalam wamesema ili kutumia uwezo huu, serikali ya Uganda inahitaji kutekeleza mageuzi. Benki ya dunia imesema ongezeko la uwekezaji wa serikali kwenye elimu na afya, linahitajika ili Uganda iweze kunufaika na ongezeko hilo la idadi ya watu.