Rais Ruto wa Kenya avunja baraza la mawaziri
2024-07-12 08:27:31| CRI

Rais William Ruto wa Kenya jana Alhamisi aliwafuta kazi mawaziri wake wote akiwemo mwanasheria mkuu, isipokuwa naibu rais na waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje na masuala ya diaspora.

Rais Ruto amesema mawaziri wapya watateuliwa baada ya majadiliano mapana kufanyika katika sekta zote.