Mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefunguliwa leo hapa Beijing.
Katika mkutano huo, Rais Xi Jinping wa China kwa niaba ya Ofisi ya Siasa ya Kamati hiyo ametoa ripoti ya kazi, na kutoa ufafanuzi wa Maamuzi ya Kukuza zaidi Mageuzi, na Kuhimiza Utimizaji wa Mambo ya Kisasa katika Pande zote kwa Njia ya Kichina.