Ghana yarekodi mlipuko wa homa ya dengue
2024-07-15 22:28:11| cri

Mamlaka za afya nchini Ghana zimesema zimethibitisha kesi 9 za homa ya dengue katika mkoa wa Mashariki nchini humo.

Mamlaka ya Huduma za Afya nchini humo (GHS) imesema katika taarifa yake kuwa, imepokea uthibitisho kutoka Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kumbukumbu ya Noguchi (NMIMR) kwamba sampuli kutoka kwa wagonjwa zimekutwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Taasisi hiyo imesema timu ya ufuatiliaji ya kitaifa imegundua ugonjwa unaofanana na malaria katika baadhi ya wilaya za mkoa wa Mashariki ambazo hazikupona kufuatia tiba za malaria zilizopendekezwa.

Pia Taasisi hiyo imesema, timu ya wataalamu kutoka ngazi ya kitaifa wameungana na timu ya kikanda kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo.