Mpango unaolenga kukuza mawasiliano kati ya watoto wa China na Afrika umezinduliwa mjini Beijing.
Sherehe ya kuwakaribisha imefanyika katika Kituo cha Watoto cha China. Makumi ya watoto kutoka Namibia, Afrika Kusini, Somalia, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekusanyika pamoja na watoto wa China. Shughuli mbalimbali zimeandaliwa kwa ajili ya watoto, ikiwa ni pamoja na michezo, uchoraji, ngoma na maonyesho ya kongfu. Katika eneo la urithi wa kitamaduni usioshikika wa kituo hicho, wametengeneza mifuko yenye harufu nzuri na vikaragosi vya kivuli, na kuhisi uzuri wa utamaduni wa jadi wa China.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wanawake wa China Bi. Huang Xiaowei amesema kuwa watoto wanabeba mustakabali na matumaini ya China na Afrika, na mawasiliano kati ya watoto yataongeza uhai mpya katika kuendeleza urafiki kati ya China na Afrika.