Rais Kagame asema Rwanda inataka kudumisha uhusiano imara na China
2024-07-15 08:22:20| CRI

Rais Paul Kagame wa Rwanda Jumamosi alisema Rwanda ina uhusiano imara na China, na inataka kudumisha uhusiano huo.

Kagame aliyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari mjini Kigali muda mfupi baada ya kumaliza kampeni yake kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge utakaofanyika Jumatatu.

Kagame alipojibu swali kuhusu uhusiano kati ya Rwanda na China katika miaka 50 iliyopita alisema, Rwanda ina uhusiano mzuri na China, na inataka kudumisha uhusiano huo. Alisema tofauti na washirika wengine, China inatendeana na Rwanda na nchi nyingine za Afrika kwa kuheshimiana, na haiingilii mambo ambayo inafikiriwa kuwa ni sahihi kwao.