Watu 35 wamefariki na wengine 250 kujeruhiwa wakati mvua kali kunyesha katika mkoa wa Nangarhar mashariki mwa Afghanistan Jumatatu alasiri na kusababisha mafuriko.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa habari na utamaduni wa jimbo la Nangarhar Qurishi Badlon, maafa hayo yaliathiri mji wa Jalalabad, wilaya ya Sukh Rod na maeneo jirani katika jimbo linalopakana na Pakistan, na kuongeza kuwa majeruhi huenda wataongezeka.
Maafa ya asili kama hayo pia yalisababisha vifo vya watu watano katika mkoa wa Kunar jirani na Nangarhar mapema Jumatatu asubuhi.
Mvua kubwa na mafuriko yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400 na maelfu ya watu kukosa makazi tangu mwezi Mei katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita.