Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina Mohammed ametoa wito kwa viongozi wa dunia kubadili mwelekeo wa rasilimali kutoka mambo ya vita hadi amani na kutimiza mapendekezo ya maendeleo endelevu.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bi. Amina Mohammed ametoa wito wa kuchukua hatua sahihi mapema ili kuokoa kuzorota kwa kutimia kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja huo, (SDGs).